23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Demokrasia iendane na mazingira-Balozi Battle

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle, amesema demokrasia ya nchi inapaswa kuendana na mazingira yake mahususi badala ya kutegemea kufanana duniani.

Akizungumza katika Mkutano wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Balozi Battle amasema kwa mfano demokrasia ya Tanzania haiwezi kufanana na demokrasia ya nchi za kifalme (kama Uingereza) na sio lazima ifafane na mifumo mingine ya kiutawala inayotumiwa na nchi nyingine duniani.

“Demokrasa ya Tanzania ni lazima izingatie muktadha na mazingira ya Tanzania, na iakisi matakwa ya watazania wenyewe. Nchi yotote duniani haina haki ya kuipangia Tanzania aina ya mfumo wake wa demokrasia,” alisema Balozi Battle.

Aidha, Balozi Battle amesema Marekani inajivunia sana hatua kubwa alizochukua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuboresha demokrasia nchini Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles