23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wanahabari tusibaki nyuma Mabadiliko ya Sheria-TEF

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutokubaki nyuma katika kushiriki kikamilifu kwenye mabadiliko ya Sheria ya Vyombo vya Habari nchini.

Wito huo umetolewa juzi Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile wakati akitoa mrejesho kwa wadau juu ya marekebisho yaliyofanywa na Serikali.

Balile alisema kuwa vipo vifungu ambavyo vimebaki katika sheria lakini Serikali imesema kuwa itavitungia kanuni huku akitolea mfano kile cha mamlaka ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.

“Tunasema kwamba katika hili la mabadiliko ya sheria ya huduma za habari umefika wakati ambao wanahabari tunatakiwa kuonyesha ushiriki wetu katika mchakato wa kanuni kuangalia kama ziko sawa.

“Sasa huu mchakato tunapaswa kuufahamu ili usije ukaendeshwa na watu ambao siyo watu wa habari, kwani kutakuwa na kanuni za kuendesha Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Vyombo vya Habari ambazo zitatungwa na waziri, pia baraza hili huru la vyombo vya habari litatunga kanuni zake za kujiendesha,” amesema Balile.

Akizungumzia mafaniko ya mchakato huo wa mabadiliko ya sheria Balile amesema kuwa kuna matokeo chanya japo ni ngumu kuyapima kwa asilimia kwa kuwa kuna baadhi ya vifungu ambavyo havikufanyiwa mabadiliko ya jumla.

“Tunaweza kusema kwamba jambo letu limeweza kusogea kwa kiasi flani japo ni ngumu kusema kwamba ni asilimia ngapi sababu kuna baadhi ya vifungu yamefanyika mabadiliko machache tu ya kanuni lakini kifungu kama kifungu hakijabadilishewa chote.

“Mfano tulikuwa tukipambana kwamba kifungu cha 35, 36 na 50a vinaanzisha jinai pia tulikuwa tunapinga kifungu cha 35 cha kukashifu Malehemu, kuna mabadiliko kadhaa hapa yamefanyika,” amesema balile na kuongeza kuwa:

“Kinachofuata baada ya kupitishwa ni marekebisho ya kanuni ambapo kifungu cha 65 kinampa Waziri mwenye dhamana kufanya marekebisho ya kanuni,” amesema Balile.

Katika eneo jingine Balile amesema kuwa kwa mabadiliko hayo kiwango cha elimu kwa waandishi wa habari kitakuwa ni Diploma.

Aidha, Balile amesema kwa sasa hakuna chombo kinachoangalia maadili katika vyombo vya habari hivyo kuna jukumu la kutengeneza maadili ya taaluma na kutakuwa na jukumu la kuangalia utendaji wa vyombo vya habari na baraza hili litakuwa na kazi ya kuamua kesi zote zinazohusu vyombo vya habari vya magazeti.

‘Hivyo utaona kwamba taaluma inakwenda kuchukuliwa na watu ambao ni waandishi wa habari, hivyo tunajukumu la kuanza kueleza jamii kwanza juu ya vyombo hivi vinavyokwenda kuanzishwa,” amesema Balile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles