32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wataalamu ngazi ya TAMISEMI wajengewa uwezo wa uelewa wa ufuatiliaji na tathmini

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeandaa Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa lengo la kutoa maelekezo katika hatua za kufuata kwenye ufuatiliaji wa afua za maendeleo.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi cha Kujenga Uelewa wa majukumu na Upimaji wa Utendaji wa Serikali ngazi ya TAMISEMI kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Anderson Mutatembwa amesema Mwongozo huo umewasilishwa katika ngazi ya Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi na Wasaidizi wa U&T ngazi ya wizara.

Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dk. Wilson Mahela akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha Kujenga Uelewa wa majukumu na Upimaji wa Utendaji wa Serikali ngazi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Machi 14, 2024..

Amesema mwongozo huo ni hatua muhimu katika kupata uelewa wa pamoja juu ya mwongozo husika na kutoa maoni kabla ya kusainiwa.

“Nisisitize kuwa, mwongozo huu umekuja wakati muafaka ambapo shughuli za U&T ndani ya idara na vitengo vyenu zinatakiwa kufanyika kwa ubora na viwango vinavyotakiwa,” amesema Mutatembwa.

Aidha, Mutatembwa ameongeza kuwa Mwongozo huo unaainisha muundo wa usimamizi na majukumu ya kila taasisi kwa ngazi za Kitaifa, Kisekta na Wizara, Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hivyo majukumu hayo yanaainisha kazi zinazotakiwa kutekelezwa ili kukamilisha upimaji wa utendaji wa kila taasisi na kuwezesha upatikanaji wa taarifa za utekelezaji na utendaji wa kila siku au pindi zinapohitajika.

“Nisisitize tena, matumizi ya Mwongozo huu yatawezesha Serikali kufuatilia, kutathmini na kupima utendaji wa taasisi zote katika ngazi za kitaifa na kisekta na kujenga msingi wa uwajibikaji wa taasisi husika kwenye mchango wa maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi,” ameongeza Mutatembwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, Sakina Mwinyimkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu amesema nivizuri kuwa na Muongozo huu ili kuweza kuwa na utendaji mzuri kwenye kazi kwa manufaa ya Serikali.

“Naomba uwepo wenu kikamilifu katika kulitimiza kusudi la kuwepo kwetu hapa leo, maana ukiangalia kwa mwaka wa fedha uliopita na huu shauku kubwa imekuwa kwenye namna ya utendaji wa serikali kwenye kuratibu na kusimamia utendaji wa serikali na ninyi wenyewe mmekuwa mashahidi tunaporudi kule kwenye utekelezaji wa kazi zetu unaona namna ambavyo tunavyofanya kazi kwa hiyo matokeo yake tunanyang’anyana rasilimali lakini tutakapo kuwa na uratibu mzuri na utekelezaji mzuri wa sera na programu hizo changamoto tutazitatua,” amesema Sakina.

Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Charlton Charles Meena akitoa wasilisho wakati wa kikao hicho.

Akifunga kikao kazi hicho Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dk. Wilson Mahela amewasisitiza watendaji kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya tamthimini zenye uhalisia wa maeneo wanayofanyia kazi kwa lengo na kuinua mapato ya maeneo yao na nchi kwa ujumla.

“Unakuta kule kwenye halmashari kwasababu tumesema ni upimaji wa serikali na vyeo mlivyopewa ni vikubwa sana na si kwamba unasimamia tu utendaji kazi wa halmashauri unakuta maafisa kilimo hawajulikani wanawajibika kwa nani unakuta wananchi wanapata shida kwa hiyo maana yangu ni kwamba ninyi mnamajukumu makubwa ya kwenda kusaidia si masuala tu ya bajeti bali na kutatua matatizo ya wananchi na mhakikishe mnaelewa hiyo miongozo yote kwa ufasaha zaidi,” amesisitiza Mahela.


- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles