27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Wataalam sekta ya ujenzi watakiwa kushirikiana katika kazi

Mwandishi Wetu

Wataalam wa Sekta ya ujenzi nchini wametakiwa kushirikiana katika kazi ili waweze be kupata tenda katika miradi mikubwa inayoendelea nchini na kuweza kushindana na wataalamu wa nje.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya malalamiko ya muda mrefu kuwa wakandarasi wazawa wamekuwa wakiachwa katika ujenzi wa miradi mbalimbali mikubwa inayoendelea nchini.

Akizungumzia na Waandishi wa habari jana Mei 19
jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa kuwajengea uwezo wataalamu wa Sekta ya ujenzi ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), chini ya udhamini wa kampuni ya JK White Cement (Africa) na Import International, Rais wa Wakadiriaji Majenzi Tanzania, Samwel Marwa amesema, ushiriano pekee ndio utakaosaidia wakandarasi kupata tenda katika miradi mikubwa nchini.

Alisema pamoja na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wakandarasi wazawa kwamba hawashirikishwi katika miradi mikubwa bado Kuna tatizo kubwa kwa wataalamu kwani wengi wanapenda kufanyika pekee yao.

“Kuna kila sababu ya wakandarasi wazawa kuona umuhimu wa kuungana pamoja ili inapotokea miradi mikubwa waweze kukidhi higezo sambamba na kuimarisha mitaji yao ili iweze kufikia malengo yanayokusudia,”alisema Marwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa AQRB, Dk.Boniface Bulamile alisema, Bodi imekuwa ikiendesha mafunzo ya aina hiyo kwa wataalamu wa fani hiyo ili kutoa elimu kwa wataalamu kuhusu vitu vipya vinavyojitokeza katika soko la ujenzi.

Do.Bulamile alisema mafunzo hayo yamekuwa yakitoa mada mbalimbali ambapo kwa mwaka huu, mada kuu ya Jana ni kujadili mikataba ya ujenzi na namna ya kuisimamia.

Naye, Mwakilishi wa wadhamini wa mafunzo hayo kutoka Kampuni ya JK White Cement, Felister Masabo alisema, Kampuni hiyo inashirikiana na Bodi kutambulisha bidhaa mpya za ujenzi zibazopatikana nchini kwa lengo la kuwezesha watanzania kuwa na Majenzi Bora.

Pia, Mdhamini mwingine kutoka Kampuni ya Import International, Ronald Moshi alisema, kampuni yao imekuwa ikishirikiana na Bodi katika shughuli nzima za kutoa elimu kwa wataalamu wa ujenzi kwa kutoa udhamini kuzingatia umuhimu wao na kazi wanazozifanya.

Alisema kampuni yao inayojishughulisha
na usambazaji bidhaa mbalimbali za ujenzi imeweza kusambaza bidhaa Bora kwa wakandarasi kupitia Ushirikiano baina yao na Bodi ambapo hadi Sasa Ina mawakala zaidi ya kumi katika mikoa Dodoma, Tanga, Arusha, Dar es Salaam na Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles