28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Daktari: Kukaa na njaa, msongo wa mawazo sio sababu za vidonda vya tumbo

TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

Daktari Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa chakula na Ini kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Dk Tuzo Lyuu, ameondoa utata juu ya vyanzo vinavyosababisha ugonjwa wa vidonda vya tumbo tofauti na wengi walivyokuwa wakifahamu

Akizungumza na MTANZANIA Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, amesema kuna sababu tatu zinazosababisha ugonjwa wa vidonda vya tumbo na kwamba Kukaa na njaa kwa muda mrefu, msongo wa mawazo na baadhi ya vyakula vilivyodhaniwa kusababisha vidonda vya tumbo havihusiani na mtu kupata ugonjwa huo.

Amesema sababu ya kwanza ni matumizi yasiyo ya lazima ya dawa za maumivu za aspirini na diclofenac bila ushauri wa daktari husababisha kupata ugonjwa huo na sababu ya pili ni kuwapo kwa bakteria aina ya H. Pylori ambao hudhoofisha kemikali zinazosaidia kulinda tindikali isiathiri tumbo.

Ameongeza kuwa sababu ya tatu ni kuwa na ugonjwa unaosababisha kulazwa  kwa muda mrefu mgonjwa hupata vidonda vinavyotokana na msongo huo, aidha kupata maumivu wakati wa njaa ama muda mfupi baada ya kula ni dalili tu ya kuwa na ugonjwa huo japo inategemea na kisababishi cha ugonjwa.

Amesema idadi kubwa ya watu wazima kuanzia miaka 50 na kuendelea wamekuwa wakikumbwa na ugonjwa huo kutokana na matumizi ya dawa za maumivu ya viungo kwa muda mrefu.

“Kuna magonjwa mengi ambayo dalili zake zinafanana na ugonjwa huo ukiwamo michubuko inayotokea katika muunganiko wa koo la chakula na tumbo(GERD), michubuko hiyo husababishwa na kulegea kwa kiunganishi hicho na hivyo kuruhusu tindikali kupanda juu,” amesema Dk Lyuu.

Amesema magonjwa mengine yanayofanana na vidonda vya tumbno ni michubuko katika tumbo la chakula(Gastritis), utumbo mdogo (duodenitis), na kupatwa na saratani ya utumbo.

Akizungumzia dalili za ugonjwa huo, Dk Lyuu amesema ni maumivu ya eneo la juu la tumbo maarufu kama chembe ya moyo, kujaa tumbo kutokana na vidonda kuchimba hadi nje ya tumbo na kuathiri mifumo mingine ya mwili pamoja na kupungua kwa damu kutokana na vidonda kuvuja damu kwa wingi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles