29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

WASICHANA 3,500 KUPEWA MBINU NDOA ZA UTOTONI

Na Jacquiline Mrisho– MAELEZO.

WASICHANA 3,738 wa mikoa ya Mara na Geita wanategemea kunufaika na mradi wa kuzuia ndoa za utotoni na ukeketaji unaofadhiliwa na Umoja wa   Ulaya (EU) na kuratibiwa na Shirika la Plan International kwa kushirikiana na mashirika ya CDF, NELICO  na Molly”s Network.

Takwimu hizo zilitolewa  jana  na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Plan – Tanzania, Gwynneth Wong wakati wa uzinduzi wa mradi huo   katika ukumbi wa ofisi za Umoja wa Ulaya,  Dar es Salaam.

Gwynneth alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikisaidiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha haki za wasichana zinalindwa na hakuna msichana atakayeachwa nyuma kwenye nyanja za maendeleo hali itakayopeleka wasichana kuwa na haki sawa na wavulana.

“Tumeona kuna haja ya kuweka mradi mwingine utakaodumu kwa miaka mitatu, wa uzuiaji wa mimba za utotoni na ukeketaji kwa mikoa ya Mara na Geita.

“Mikoa hiyo imeonekana kuongoza kwa matatizo hayo hivyo tunaushukuru Umoja wa Ulaya kwa kutoa Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya kuendeshea mradi huu,” alisema. Gwynneth.

Alisema takwimu za mwaka 2016 za Utafiti wa Demographia na Afya zinaonyesha kuwa ndoa za utotoni mkoani Mara ni asilimia 55 na kwa Geita ni asilimia 37 na ukeketaji kwa Mkoa wa Mara ni asilimia 32 kwa asilimia za  taifa, hivyo ni lazima kuanza na maeneo yaliyoathirika zaidi.

Balozi wa Umoja wa Ulaya, Roeland Van de Geer alisema umoja huo unatambua nafasi ya msichana katika jamii na nafasi ya baadhi ya mashirika yanayoshirikiana na Serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kuhakikisha haki sawa kwa wote.

“Sisi tunatoa fedha lakini nyie ndiyo watendaji hivyo tunawashukuru sana, lakini pia tunatakiwa tutambue kuwa maendeleo ya kudumu hayawezi kupatikana kwa kuwaacha wanawake nyuma kwa maana hiyo tunatakiwa tufanye juhudi za kuhakikisha tunaenda pamoja,” alisema Balozi  Roeland Van de Geer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles