26.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

APANDISHWA KIZIMBANI KWA UTAPELI WA MIL 20

Na CAROLINE CHALE (TUDARCO)

-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Goba,  Dar es Salaam, Marten Nyetika(49), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, akikabiliwa na shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Shadrack Mwamakolia.

Mbele ya  Hakimu Mkazi Mfawidhi, Frank Moshi, Wakili wa Jamhuri,  Ramadhani Mkimbu alidai tukio hilo lilitokea Machi 4, 2016, Wilaya ya Kinondoni, ambako mtuhumiwa alijipatia   Sh milioni 20 kwa ajili ya mauziano ya eneo wakati halikuwa lake.

“Mshtakiwa unatuhumiwa   kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,   Sh milioni 20 kutoka kwa  Mwamakolia kwa ajili ya mauziano ya eneo ambalo ulitambua fika kuwa halikuwa mali yako jambo ambalo ni   kinyume cha sheria,” alisema Wakili Mkimbu.

Mtuhumiwa alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana hadi Septemba 18, mwaka huu itakapotajwa tena.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,263FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles