25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KUUA WAKE ZAKE

gavel

Na WALTER MGULUCHUMA-Katavi

MAHAKAMA Kuu ya Sumbawanga, imewahukumu watu wawili kunyongwa hadi kufa katika kesi mbili tofauti baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wake zake wawili kwa kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Sumbawanga, Adamu Mambi.

Katika kesi ya kwanza, Mahakama Kuu, ilimhukumu mkazi wa Kijiji cha Mamba, wilayani Mlele aitwaye Shija Sosomo, kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana  na hatia ya kumuua kwa makusudi mke wake mkubwa kwa kumchinja baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi akimtuhumu kumuua mtoto wake mdogo kwa ushirikina.

Awali, kwenye kesi hiyo, mwendesha mashitaka, Achiles Mulisi, alidai mahakamani hapo, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, Januari 23 mwaka 2012 katika Kijiji cha Mamba.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo hiyo, mshitakiwa Shija Sosomo, alimchinja mke wake mkubwa, Mwashi Nkuba baada ya kumtuhumu kuwa amemuua kichawi mtoto wake wa mke mdogo.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa, mshtakiwa baada ya kufanya mauaji hayo, alikwenda  kutoa  taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi na kumweleza kuwa amemuua mke wake.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mambi aliiambia mahakama hiyo, kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Naye Mwanasheria wa Serikali, Achiles Mulisi, aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Katika kesi nyingine, Mahakama Kuu ya Sumbawanga, ilimhukumu kunyongwa hadi kufa, Monde Ndushi (52), mkazi wa Kijiji cha Chamalendi, wilayani Mlele, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake kwa makusudi.

Mwendesha Mashtaka, Jamila Mziray, aliiambia mahakama hiyo, mshtakiwa alitenda kosa hilo, Machi 12, mwaka  2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles