24.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

WASHAURI WA TRUMP WADAIWA KUTUMIA BARUA PEPE BINAFSI

NEW YORK, MAREKANI


WASHAURI sita wa karibu wa Rais, Donald Trump wamekuwa wakitumia barua pepe binafsi kuzungumzia masuala yahusuyo Ikulu ya Marekani tangu Trump aingie madarakani, linaripoti Gazeti la New York Times.

Gazeti hilo la hapa limeyataja majina ya washauri hao na mtoto wake Ivanka kuwa miongoni mwao.

Aidha Jarida la Newsweek limeandika kuwa barua pepe alizokuwa anazitumia Ivanka zililenga kutafuta ushirikiano na kampuni za kibiashara na aliwatumia nakala wakuu wawili wa Ikulu.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, rais Trump alitishia kumfunga mpinzani wake Hillary Clinton baada ya kubainika alitumia barua pepe yake ya binafsi wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Na siku ya jumapili, mume wa Ivanka, Jared Kushner alitajwa pia kutumia barua pepe binafsi katika shughuli za kiserikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles