28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

AMBER LULU AWAVUTIA KASI MASTAA WA KIKE

Na JESSCA NANGAWE


MSANII aliyeangukia katika muziki wa Bongo Fleva, Lulu Mkongwa ‘Amber Lulu’, anayetamba na wimbo wake wa ‘Watakoma’, amewataka wasanii wa kike katika muziki huo kujipanga, la sivyo atawapoteza.

Amber Lulu, aliyekuwa Video Vixen, ameliambia MTANZANIA kuwa, hatishwi na kasi ya wasanii hao ambao kwa sasa wana majina, badala yake yupo kwa ajili ya kuleta upinzani na kuchukua nafasi zao.

“Ninachowaambia wasibweteke, kwani nimekuja kuwapoteza kimuziki, nimehamia huku baada ya kuona ninaweza na nimejipanga kufanya vizuri zaidi ya nilipotoka, natarajia mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wangu na ukweli watambue sijavamia fani,” alisema.

Amewataka wasanii wenzake wanaong’ang’ania kwenye ‘game’ na wasiotaka watu wapya watambue wao wana vitu vipya ambavyo wanatamani vionekanane ndani ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles