29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

KYLIE AWAACHA NJIAPANDA MASHABIKI

NEW YORK, MAREKANI


MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kylie Jenner, amewaacha na maswali mengi mashabiki wake baada ya kuposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram ambayo inaonesha hakuna dalili ya kuwa na ujauzito.

Mapema mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba staa huyo ana ujauzito na hata mama yake alithibitisha kuwa mwanawe ana ‘kibendi’.

Picha ambayo ameiweka mwanamitindo huyo inaonesha akiwa na tumbo dogo na kuacha swali kwa mashabiki wake kwamba ‘Nina mimba?’ Hata hivyo, picha hiyo iliyowekwa ilikuwa ya zamani, lakini bado iliwachanganya mashabiki.

Taarifa za kuwa na ujauzito zilisema kwamba, mrembo huyo anatarajia kuwa na mtoto wake wa kwanza Februari, mwakani, lakini yeye mwenyewe hajataka kuthibitisha kama kweli ana ujauzito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles