29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

T.I, TAMEKA HARRIS WARUDIANA

CALIFORNIA, MAREKANI


RAPA Clifford Harris ‘T.I’ na mama wa watoto wake, Tameka Harris, wamethibitisha kurudiana baada ya miezi kadhaa kusambaa taarifa kuwa wamepeana talaka.

Taarifa za awali zilisema kuwa, mrembo huyo aliamua kuomba talaka kutokana na baba watoto wake, T.I, kuwa mwongo kwenye mapenzi, lakini wameamua kukaa chini na kumaliza tofauti zao.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya familia hiyo, wawili hao wamedai mapenzi ya kweli hayawezi kujificha, hivyo japokuwa walitofautiana, lakini wameweza kuweka sawa na kukubaliana baadhi ya mambo.

Hata hivyo, wawili hao wamedai kuwa, vyombo vya habari vilichangia mgogoro wao, hivyo kwa sasa wapo kwenye mikakati mipya ya kuyafanya mapenzi yao kuwa ya siri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles