24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

WAHAMIAJI WA LORI LA DANGOTE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Dereva wa lori la Kiwanda cha Saruji cha Dangote,  Khalid Sadik na wenzake wawili wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia lori hilo kusafirisha wahamiaji haramu wanane raia wa Ethiopia.

Mshtakiwa Sadik, kondakta Hussein Hassan, Jumanne Mtambo na raia hao wa Ethiopia wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka matano mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

Wakili wa Idara ya Uhamiaji, Novatus Mlay aliwataja washtakiwa ambao ni raia wa Ethiopia kuwa ni Solomon Ertiso, Gezahegn Tiroro, Haile Latso, Thadeus Lilanso, Dawit Kuruse, Dezret Godebo,  Firaru Hadago na Elioj Akola.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, Septemba 20, mwaka huu maeneo ya Mbagala Korogwe na Mtongani, jijini Dar es Salaam ambapo raia waliingia na kukutwa nchini bila kibali.

Inadaiwa raia hao wa Ethiopia siku hiyo, kwenye maeneo hayo, waliingia na kukutwa nchini bila ya kibali na kwamba Watanzania hao ambao ni washtakiwa pia walikutwa wakiwasafirisha wahamiaji hao haramu kwa kutumia  Semi Trailer namba T. 181 DKB likiwa na tela lake namba T 961 DKA mali ya Dangote Cement Limited ambao waliingia nchini kinyume cha sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles