Wasanii Tanzania waikataa Cosota

0
806

MWANAFA-NEWNA KHABIBU NASSORO, (MUC)

WASANII wa muziki nchini wameukataa uongozi wa Cosota kutokana na usimamizi mbaya wa kazi zao.
Wakizungumza na waandishi wahabari katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Little Theatre, jijini Dar es Salaam jana, walisema hawana imani na uongozi wa Cosota na kampuni ya kusimamia kazi za wasanii Afrika Mashariki (CMEA).
“Hatuna imani na Cosota, CMEA na Basata kutokana na kushindwa kusimamia kazi zetu.
“Hata mchakato uliotumika kupata viongozi wa mashirikisho hayo si sahihi kwa upande wetu kwa kuwa viongozi waliopo ndani ya uongozi huo hakuna hata mmoja ambaye ni msanii,” alisema Mwana FA.
Mbali na hayo, wasanii hao wanatarajia kupeleka malalamiko yao kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here