Drake awakutanisha Lil Wayne na Birdman

0
971

Wimbledon 2015 - Day 1 - Celebrity SightingsMIAMI, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Lil Wayne na Birdman, wamekutana kwa mara ya kwanza kwenye ‘party’ ya msanii mwenzao, Drake.

Wawili hao wana mgogoro tangu Agosti mwaka jana hivyo kuwafanya wavunjeukaribu wao, lakini mwanzoni mwa mwaka huu wawili hao wamejikuta wakikutana katika pati ya Drake ambayo aliiandaa kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya.

Pati hiyo ilifanyika mjini Miami kwenye Ukumbi wa E11, hata hivyo mashabiki wamebaki na maswali mengi kama wawili hao wamemaliza tofauti zao.

Katika pati hiyo kulikuwa na wasanii mbalimbali ambao walijitokeza na kupiga picha ya pamoja huku Lil Wayne akionekana kuwa karibu na bosi wake wa zamani, birdman.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here