27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Future amshambulia Ciara

futureNEW YORK, MAREKANI

MSANII wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nayvadius Wilburn ‘Future’, amemshambulia mpenzi wake wa zamani, Ciara kwa malezi mabaya ya mtoto wao.
Wawili hao walifanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye walimpa jina la Future Zahir, wakati wa uhusiano wao, lakini baada ya kutengana mtoto huyo akawa anaishi na mama yake ‘Ciara’ ila Future ameonekana kuchukizwa na malezi ya mama huyo kwa mtoto wake.
“Najua mwanangu anateseka kukaa na mama yake, hafundishwi maadili mazuri hivyo ninaamini anapotea, hii yote ni kutokana na Ciara kung’ang’ania mtoto huyo ila ni bora angekuwa anakaa kwangu,” alisema Future.
Hata hivyo, sio mara ya kwanza Future kumshambulia mpenzi huyo, ambapo Julai mwaka jana aliwahi kumwambia kwamba anamfundisha mabaya mtoto huyo kwa kuingia na mchumba ndani ya nyumba yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles