24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

WASAA YATAKA WANAWAKE KUWEKEZA KWENYE VIWANDA

Na George Mshana,

ASASI isiyo ya Kiserikali inayoshughulika na wanawake wajasiriamali wanaofanya kilimo-biashara katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara (Wasaa), inawataka wanawake na vijana wanufaike na uchumi wa kati kwa kutumia fursa zilizopo kwa kuwekeza kwenye sekta ya viwanda.

Hayo yamesemwa na Rais wa Wasaa, Margaret Chacha, katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam wiki hii.

“Wasaa itawaelimisha wanawake na vijana wanaofanya kilimo-biashara na kuwaunganisha na masoko. Ni wakati wa vijana na wanawake kuwa na maendeleo ya kiuchumi. Wachukue fursa ya kuwekeza kwenye viwanda,” anasema Chacha.

Wasaa wanataka mfugaji afuge kitaalamu. Wanawake na vijana wanufaike kwenye uchumi wa kati. Tuna mtandao ambao utawaunganisha na viwanda.

“Tuna madhumuni ya kufungua matawi mikoani. Tunataka mwanamke aweze kumiliki ardhi na mali nyingine ili aweze kujikomboa kiuchumi. Wasaa inataka kuwasaidia wanawake wapeleke mazao yao nje ya nchi. Tuna fursa kubwa, tuna ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo. Watu waangalie kilimo kama njia ya kujiajiri.

 Wasaa itawaunganisha watu na Saccos ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kuanzisha miradi midogo midogo itakayowaingizia kipato na kuboresha maisha yao. Wanawake na vijana ndio wataleta maendeleo ya viwanda na uchumi wa kati,” anasema.

“Wasaa iliandikishwa mwaka 2012. Tumeona tuwawezeshe wanawake waweze kuingia kwenye uchumi wa kati. Wananchi wenye viwanda waweze kuuza mali zao. Maghala ya kuhifadhia chakula yawepo.

“Kilimo kipo Dar es Salaam na mikoani, tunawakwamua wale waliopo mikoani. Wasaa inaangalia mbegu bora, ukulima bora wenye tija. Tuna nguzo tatu; uchumi, maendeleo ya jamii, mazingira na utumiaji mzuri wa maji,” anasema Chacha.

Kwa upande wake, Veronica Urio, mkulima wa Morogoro, anasema changamoto kubwa wanayoipata wakulima ni masoko, unakuwa na bidhaa lakini huna mahali pa kuuza.

“Wasaa inaniunganisha na masoko. Tunalima matikiti, mbogamboga, nyuki, na tunachimba visima,” anasema.

Naye Wanne, Mjasiriamali kutoka Dar es Salaam, anasema: Wasaa inatusaidia kupata malighafi, tukipata malighafi ya pamba kwa bei ya juu na bidhaa zetu zinakuwa bei ya juu na hivyo zinashindwa kukabiliana na ushindani katika soko.

“Tunaishukuru Wasaa kwa kutuunganisha na Saccos ili tuweze kukopa na kuanzisha miradi ya kutuingizia kipato ambayo itatusaidia kukabiliana na umasikini. Taasisi  hii ina mikakati ya kuwa na wawakilishi ambao ni kama wakala mikoani kama Morogoro, Mbeya na Mwanza. Tutafanya makongamano mengi mikoani, kwa kutumia ofisi ya Wasaa Uganda na Zambia na Malawi itasaidia wanawake waweze kutimiza mahitaji yao ya oda,” anasema Wanne.

Tumejipanga kutoa mitaji, kumwezesha mwanamke na kijana kuweza kukopesheka bila kuwa na haja ya kuwa na dhamana.

Veronica Urio anasema wakinamama na akinababa wafanye kilimo ili kuweza kupata maendeleo ya kiuchumi na itawasaidia pia wasipate maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, kwa sababu watakuwa wanajishughulisha na kilimo na hivyo mawazo yao yatakuwa kwenye shughuli hiyo na hawatakuwa na muda wa kufikiria mambo ambayo yanaweza kusababisha kupata maambukizi ya ukimwi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles