30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

SPIKA AKATAA TRUMP KUHUTUBIA BUNGE UINGEREZA

Spika wa bunge la Uingereza John Bercow amepinga hatua ya Rais Donald Trump kuhutubia bunge la taifa hilo wakati wa ziara yake.

Hii ni kwa madai kwamba matamshi yake yamesababisha chuki huku mbunge mmoja akisema kuwa hayafai huku wengine wakidai hafai kupendelea upande mmoja.

Bercow alisema pingamizi dhidi ya ''ubaguzi wa rangi na ule wa kijinsia'' zinapaswa kuangaziwa sana na wanachama wa bunge hilo.

Akizungumza bungeni siku ya jumatatu, Bercow alisema kuwa anapinga Rais Trump kuhutubia mabunge yote kama ilivyo ada na viongozi wengine wa kimataifa na kuongeza kusema kuwa  kulihutubia bunge sio haki bali ni heshima anayopewa kiongozi wa kimataifa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa maswala ya kisiasa Eleanor Garnier, hilo ni pigo la kidiplomasia kwamba rais Trump hataruhusiwa kuhutubia bunge la nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles