22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

WARUNDI WAKATWA MISHAHARA KUCHANGIA UCHAGUZI MKUU 2020

BUNJUMBURA, BURUNDI


WAFANYAKAZI wa umma nchini Burundi wameanza kukatwa mishahara ili kutunisha hazina ili kugharimia Uchaguzi Mkuu utakaofayika mwaka 2020.

Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, raia wote wa Burundi walio na zaidi ya umri wa kupiga kura wa miaka 18 na zaidi wanatakiwa wachangie katika hazina hiyo ya Taifa.

Serikali ya Burundi imesema imechukua uamuzi huo ili kuziba pengo lililosababishwa na uamuzi wa wafadhili kuzuia misaada tangu mzozo wa mwaka wa 2015 wakati Rais Pierre Nkurunziza alipowania kwa muhula wa tatu.

Hata hivyo, Serikali imedai hazina hiyo ya uchaguzi ni wazo la raia wa Burundi wenyewe, kauli, ambao imepingwa vikali na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Vyama hivyo, havijafurahishwa na uamuzi huo wa kuwashurutisha raia kulipa ushuru na kufadhili uchaguzi.

Wamesema wanapanga kuwasilisha malalamiko yao kwa Tume ya Taifa ya Majadiliano ili kutatua mzozo huo.

Awali vyama hivyo viliitisha mazungumzo na serikali kuhusiana na suala hilo na hadi sasa hilo halijatendeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles