22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

CHINA YAISHUTUMU MAREKANI KUENDELEZA SILAHA ZA NYUKLIA

BEIJING, CHINA


SERIKALI ya China imeitaka Marekani kuachana na fikra ya ‘vita vya baridi’ baada ya Washington kutangaza mpango wa kupanua silaha za nyuklia kwa kuunda mabomu madogo.

“Nchi inayomiliki silaha kubwa za nyuklia duniani, inapaswa kuongoza juhudi za kupunguza badala ya kwenda kinyume,” Wizara ya Ulinzi ya China ilisema jana.

Jeshi la Marekani linaamini silaha zake za nyuklia zinaonekana kubwa kustahili kutumika na sasa inataka kutengeneza mabomu madogo.

Limeitaja China, Urusi, Korea Kaskazini na Iran kama mataifa yanayoweza kuwa tishio kwake.

Nyaraka iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani siku ya Ijumaa- inayojulikana kama Nuclear Posture Review (NPR), inadai  kutengeneza silaha ndogo za nyuklia kutasaidia kupambana na fikra kuwa Marekani si tishio tena.

Ingawa silaha hizo ndogo hazina nguvu kubwa, bado zinaweza kusababisha madhara.

Sababu kubwa ya kuidhinishwa mpango huo mpya kukabiliana na kile kile kilichodaiwa ‘tishio linaloongezeka la mataifa yenye yenye nguvu’ kama China na Urusi.

Urusi kwa upande wake ilishaishutumu Marekani kwa kuchochea mashindano ya silaha za maangamizi na imesema itachukua ‘hatua zipasazo’ kuhakikisha usalama wa Urusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles