WAPINZANI WATAKA RAIS APUNGUZIWE MAMLAKA

0
520
Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Na KULWA MZEE-DODOMA

WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wamependekeza Rais apunguziwe mamlaka katika umiliki wa maliasili za nchi.

Wamesema kama akitokea Rais asiyekuwa mwaminifu, nchi inaweza kuangamia kupitia sheria za madini zinazotarajiwa kupitishwa.

Hayo yalielezwa jana na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) wakati akichangia hoja katika Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 na Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.

“Mjadala huu muhimu unatengeneza sheria kuhusu rasilimali zetu, lakini ushabiki katika kutunga sheria umekuwa muhimu kuliko sheria yenyewe.

“Tulipitisha sheria ya utakatishaji fedha ambayo ilionekana inatungiwa upande mmoja, lakini leo sheria ile inakula watu wa upande wao.

“Ukisikiliza hotuba ya Rais analalamikia uongozi uliopita pamoja na Bunge, kwamba lilifanya makosa katika kutunga sheria, yaani Rais analalamika kwa kutunga sheria mbaya.

“Kwa hiyo, kama tuko makini, katika kubadili sheria ni vema muswada ungekuwa wa kuondolea kinga viongozi wanapokuwa madarakani,” alisema Heche.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), alisema kazi wanayofanya ni muhimu, lakini aina ya mjadala walionao haulingani na uzito wa jambo lililopo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here