27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RUGEMALIRA, SETHI WAONGEZEWA MASHTAKA

Watuhumiwa wa kesi ya utakatishaji fedha ya IPTL, Harbinder Sethi na James Rugemalira, wakipanda gari la Magereza kurudishwa gerezani baada ya kutoka kuongezewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana. PICHA: IMANI NATHANIEL

Na NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya Independent Power Limited (PAP), Habinder Sethi Sigh na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira wameongezewa mashtaka sita ya kutakatisha fedha haramu.

Awali walishtakiwa kwa makosa sita yakiwamo ya kuhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali lakini mashitaka hayo sasa yameongezwa na kufikia 12.

Kesi hiyo ilitajwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, uliwasomea upya mashitaka.

Wakili huyo alidai kuwa katika mashitaka ya kutakatisha fedha haramu, kati ya Novemba 29, 2013 na Januari 23, 2014 jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao walikula njama za kutakatisha Sh bilioni 309.5 za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) huku wakijua kwamba upatikanaji wa fedha hizo ilikuwa ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Katika shtaka la nane linalomuhusu Sethi, ilidaiwa kuwa Novemba 29, 2013 katika tawi la Kati la Benki ya Stanbic, alijipatia kutoka BoT Dola za Marekani 22,198,544.60.

Shtaka la tisa pia linamuhusu Sethi ambapo ilidaiwa kuwa kati ya Novemba 29, 2013 na Machi 14, 2014 katika tawi la Kati la Benki ya Stanbic, Kinondoni alijipatia kutoka BoT Sh 309, 461,300,158.27.

Wakili huyo alidai kuwa katika shtaka la 10, Rugemarila anadaiwa kuwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St. Joseph, alijipatia Sh 73,573,500,000 kutoka kwa Sethi huku akijua kwamba upatikanaji wa fedha hizo ilikuwa ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Shtaka la 11 pia linamuhusu Rugemarila ambapo ilidaiwa kuwa Januari 23, 2014 katika Benki ya Mkombozi tawi la St. Joseph alijipatia kutoka kwa Sethi Dola za Marekani 22,000,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles