31.9 C
Dar es Salaam
Sunday, January 16, 2022

Wapiga kura kuwataja watuhumiwa mauaji ya watoto Simiyu

Derick Milton, Busega

Wananchi wa Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo wamepiga kura ya siri ya kuwataja watuhumiwa wa mauaji ya watoto wilayani humo.

Hatua hiyo inatokana na maazimio ya wananchi hao na katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Jumanne wiki hii baada ya wananchi hao kusema hawana imani na polisi kutokana na kuwakamata wanaodhaniwa kuwa watuhumiwa kisha kuwaachia na kuwaacha watuhumiwa halisi wa matukio hayo.

Zoezi la kupiga kura lilianza leo saa 5:02 asubuhi na kumalizika saa 7:34 mchana, huku likisimamiwa vema na Mtaka.

“Zoezi limekamika, sasa kura zinapelekwa Bariadi kwa ajili ya kuhesabiwa. Watakaohusika na kuhesabu ni Magereza, Usalama wa Taifa, Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa), JKT ( Jeshi la Kujenga Taifa) na Idara ya Uhamiaji.

“Polisi hawatahusika katika kuhesabu kwa sababu wanatuhumiwa kuhusika na matukio hayo,” amesema Mtaka.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,603FollowersFollow
530,000SubscribersSubscribe

Latest Articles