31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Lulu kugawa misaada kwa watoto yatima Iringa

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu amezitangaza sehemu ambazo ataenda kutoa msaada wa nguo, vyakula na mahitaji mbalimbali kupitia kampeni yake ya ‘Save My Valentine’ ambavyo ni vituo vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira vya Faraja House na Tosamaganga Orphanage Center vya mkoani Iringa.

Lulu alianzisha kampeni ya Save My Valentine Januari 23, mwaka huu kwa kuuza baadhi ya nguo zake 67 lakini pia aliwaomba mashabiki wake na watu wengine ambao wameguswa kuchangia fedha na mahitaji mengine muhimu kwa binadamu.

Akizungumza leo Alhamis Februari 14 ikiwa ni kilele cha kupokea michango kwa ajili ya kampeni hiyo, Lulu amesema amechagua vituo hivyo vya Iringa kutokana na utafiti mdogo alioufanya amegundua ni mkoa wenye idadi ya watoto yatima wengi na wanaoshi katika mazingira magumu.

Lulu pia amezielezea sababu kuu za kuvichagua vituo hivyo ukiachilia mbali changamoto za kimkoa lakini amezitaja sababu binafsi ya kuvichagua kuwa sehemu yake ya kusherehekea siku ya wapendanao na watoto wenye uhitaji.

“Kituo cha Faraja House kilianzishwa mwaka 1997 na kwa muda wote kimelea watoto ambao wamesoma na kuhitimu katika taaluma mbalimbali ila miezi kadhaa iliyopita kilipata ajali ya moto na kuteketeza majengo na samani, pamoja na changamoto ila wamefanya jitihada za kujenga mengine japo hayajakamilika.

“Na Tosamaganga Orphanage Center ni kituo ambacho kinalea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu ila kituo hiki kina zaidi ya watoto 60 ambao wana umri kuanzia siku Mona hadi miaka mitano na wengi wao mama zao walipoteza maisha wakati wa kujifungua au wametelekezwa na wazazi lakini ni wadogo sana,” ameelezea Lulu huku akibubujikwa na machozi.

Aidha Lulu amewashukuru mashabiki zake na watu wote waliojitolea kumchangia katika kampeni yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles