23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Ambokile: Nasubiri baraka za kocha ili nicheze

Lulu Ringo, Dar es salaam

Mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City, Eliud Ambokile aliyetolewa kwa mkopo katika klabu ya Black Leopard ya Afrika Kusini amesema kwa sasa anasubiri baraka za kocha kama atafaa kwenye mfumo wake ama la ili aanze kuchezea klabu yake mpya.

Eliud amesajiliwa katika klabu ya Black Leopard kwa mkopo wa miezi mitatu baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kuisha. Alikua bado hajaanza kucheza kutokana na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutopatikana.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Februari 14 Eliud amesema Hati hiyo imepatikana jana na kilichobaki kwake ni kujituma kwa bidii ili aendane na mfumo wa kocha aweze kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

“Nashukuru Mungu kibali cha kazi kimetoka jana kikubwa kilichobakia nikujituma kwa hali na mali niweze kumfuraisha kocha anipatie nafasi ya kucheza maana tamaa yangu kubwa nikuhakikisha nacheza hapa bila kushindwa,” amesema Ambokile.

Timu ya Black Leopard inanolewa na Kocha,Dylan Kerr aliyewahi kuwa kocha wa kikosi cha Gor Mahia ya Kenya na Simba ya Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles