WASHIRIKI kutoka Dar es Salaam, Greylove Mwidunda, Sarah Jackson na Nassor Amry pamoja na mshiriki kutoka Mkoa wa Mbeya, Bezalel Nataaniel, wameaga shindano la kusaka vipaji vya wanamuziki Bongo Star Search (BSS).
Kutolewa kwa washiriki hao wanne kumefanya shindano hilo libakiwe na washiriki 15 wanaoendelea na kambi.
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen, alisema washiriki waliotolewa walikuwa na kasoro ndogondogo katika uimbaji ikilinganishwa na washiriki waliobakia.
“Washiriki wote ni wazuri lakini hili ni shindano anayeteleza hana budi kuondoka kupisha wengine wenye uwezo zaidi,” alisema Ritha.