29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Diamond, Sauti Soul wafanya kweli Mauritius

sauti solNA MWANDISHI WETU

MKALI wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ na wakali wa Afro Pop kutoka Kenya wanaounda kundi la Sauti Sol, wamefanya onyesho kabambe katika hitimisho la Tamasha la 2015 Content Showcase Extravaganza, lililofanyika visiwa vya Mauritius.

Onyesho hilo lililofanyika katika hitimisho la wiki ya furaha, burudani na mafanikio makubwa kwa Kampuni ya MultiChoice Africa, liliwakutanisha waandishi zaidi ya 90 kutoka kote Afrika, wasanii mashuhuri na watu maarufu waliokutana katika visiwa hivyo.

Katika onyesho hilo Diamond, Sauti Sol na Mnigeria ambaye ndiye wa kwanza kufanyakazi chini ya usimamizi wa VP Records, walionyesha uwezo mkubwa wa kulitawala jukwaa na kufanya ambavyo mashabiki wao walitarajia kutoka kwao.

Hafla ya uzinduzi wa tamasha hilo lililokuwa na dhumuni la kuonyesha maudhui yaliyopo kwenye ving’amuzi vya DStv lililohitimishwa juzi, lilifanyika kwenye hoteli ya Outrigger Resort ambapo msanii kutoka Nigeria, Mr Flava alitumbuiza huku mastaa wengine akiwemo, Genevieve Nnaji, Ramsey Nuoah, Rita Dominic na Desmond Elliot wakimshuhudia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles