25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Wanawake watakiwa kujitosa usafirishaji

Na BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM

WANAWAKE wametakiwa kutoogopa na kuondokana na dhana ya kukwepa kuchukua masomo ya sekta ya usafirishaji wa vyombo vya moto, wakidhani kuwa ni kwa ajili ya wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani,  ambayo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka, Mkurungezi wa Taasisi ya kutetea haki za wanawake mabaharia nchini, Kapteni Dilshad Murtaza alisema jamii imejenga utamaduni wa kuwa wanaofanya kazi hiyo ni wanaume tu jambo ambalo sio la kweli.

Alisema wanawake wanayonafasi kubwa ya kufanya kazi hiyo kwani wao pia ni miongoni mwa wasomi waliosomea masomo hayo.

“Sekta ya usafirishaji ni nyeti ambayo katika jamii pia imekuwa ni ngumu kuona wanawake wakishiriki katika kazi hasa za uendeshaji wa vyombo vya majini.

“Katika sekta hii mwitikio wa wanawake ni awali ulikuwa ni mdogo, lakini kwa sasa hali imebadilika kwa dunia ya sasa mwitikio umekuwa mkubwa sana watu wanauwelewa hawachagui kazi,” alisema.

Kwa upande wake, mwakilishi wa maofisa wa kazi kutoka moja ya vyama vya maofisa kazi vilivyopo nchini ya Shirika la Usafirishaji Ulimwenguni (ITF) Nice Mwansasi alisema sekta hiyo imekuwa ikikubwa na chagamoto nyingi ikiwemo soko la ajira kuwa dogo.

Alisema kutokana na chagamoto hiyo ni vema serikali ikaweka mitaala mashuleni ili kuweza kuweka mwitikio katika jamii.

“Tunaiomba serikali iweke mkazo kwa kuweka mitaala mashuleni inayohusu sekta ya usafirishaji ili muweza kuamasisha vijana kupenda kufanya kazi hiyo,” alisema Nice.

Pia aliongeza kwa kuzitaka  Asasi za kiraia kujitokeza na kuwahamasisha wanawake kuwa sekta ya usafirishaji inafursa nyingi na inalipa wahache kukaa majumbani na kufanyakazi kupitia sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles