27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kugawa mapori kwa wafugaji

Na CLARA MATIMO – MISUNGWI

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ametangaza neema ya kugawa mapori kwa wafugaji ili wapate maeneo mazuri ya kufugia mifugo yao.

Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Misungwi akiwa kwenye ziara ya kuwanadi wagombea wa chama hicho Mkoani Mwanza katika uwanja wa Amani.

Alisema pia Serikali itachimba mabwawa katika mapori hayo itaweka  maabara, kliniki na dawa za mifugo ili kuhakikisha wafugaji wanapata huduma zote muhimu kwa ajili ya kuhudumia mifugo yao.

Alisema neema hizo zote watanufaika nazo endapo watachagua wagombea wa CCM wakiongozwa na mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk John Magufuli kwa kuwa anauwezo wa kuongoza na kusikiliza changamoto za wananchi kisha anazitatua.

”Tayari tumekwisha tenga mapori hayo na mipangp yote ya kuweka mabwawa , kliniki na dawa inaendelea, lakini baadhi ya wafugaji wamekwishaanza kupata ruzuku.

“Dawa za mifugo tutazitoa kwa gharama ndogo kama dawa inauzwa Sh 20,000 mfugaji atauziwa kwa Sh 10,000, CCM ndiyo chama pekee kinachowafuata wananchi wake na kuzungumza nao ili kujua changamoto zao kisha tunazitatu,” alisema.

Alisema kwa upande wa wavuvi tayari wamekwishaondoa kodi kwenye zana za uvuvi   pia wamepunguza ushuru kwa wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi.

“Katika kuboresha sekata ya uvuvi, kilimo na mifugo tumeanzisha viwanda vya mazao hayo ili wananchi wote wanaojishughulisha na shughuli za uzalishaji katika sekata hizo, ndugu zangu kiongozi pekee anayeweza kuyasimamia vizuri mambo haya ni Dk Magufuli.

 “Wachimbaji wadogo nao tumewajali ekari zaidi ya 28,000 tumezigawa kwa wachimbaji wadogo na masoko ya kuuzia rasilimali hizo yapo hapa nchini saizi hawaibiwi kabisa, ndugu zangu naomba kura zenu za kutosha kwa wagombea wetu,” alisema.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Misungwi kwa tiketi ya CCM, Alexander Mnyeti, alimuomba Waziri Majaliwa kuwajengea barabara ya kutoka wilayani humo kupitia Kahama Mkoani Shinyanga kisha nchini Rwanda na Burundi kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.

Baada ya kuzungumza na wananchi wa Jimbo la Misungwi alikwenda Jimbo la kwimba na   Sumve ambapo akiwa Kwimba aliahidi wananchi wa jimbo hilo ambao wengi ni wakulima kwamba wakichagua wagombea wa CCM watawajengea soko bora  kwa ajili ya kuuzia mazao yao.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles