23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE WALIA TATIZO LA MAJI  

 

Na ANNA RUHASHA


WANAWAKE wa Kata ya Nyamapande wilayani  Sengerema   wamelalamikia tatizo la uhaba wa maji kwa  kulazimika kuyafuata mbali jambo ambalo limekuwa likihatarisha ndoa zao.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wenzake, Leticia Francis alisema wamekuwa wakilazimika kuamka saa 6.00 usiku na  kuvizia maji visimani hivyo kuwaacha waume zao wamelala na kukaa huko saa nane wakisubiri kuchota maji.

Kwa mujibu wa wananchi hao,  jambo hilo limeanza kuzua migogoro katika ndoa zao.

“Hili limeleta taabu sana baadhi yetu wamekuwa wakipigwa na waume wao wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya mapenzi kwa kisingizio cha kufuata maji.

“Ni tatizo kubwa kwa wanawake tunawaacha watoto na waume zetu na siku nyingine unakwenda nakukosa maji pia kwa kuwa wahitaji ni wengi hivyo kisima kinazidiwa uwezo,” alisema.

Diwani wa Kata ya Nyampande, Kaswahili Goerge (CCM) alikiri kuwapo  changamoto ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo.

Alisema  wamekuwa wakitegemea visima viwili virefu vya maji ambavyo ni mali ya watu binafsi.

Alisema walikwisha kuwasilisha jambo hilo kwa mkugugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na imani yake ni kuwa hatua zimeanza kuchukuliwa kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji.

“Tatizo la maji hapa nikubwa kuliko yote, kuna visima viwili tu vinavyohudumia  pia  halmashauri imeanza kutuletea maji kwa kutumia boza na matanki yapo wananchi waweze kununua kwa ndoo sh 50 ili kupunguza changamoto za kuvunjika kwa ndoa,” alisema Kaswahili.

Alisema serikali katika  bajeti   ya mwaka 2017/2018 imepanga kuanza kusambaza mabomba ya maji kutoka kwenye mradi mkubwa wa maji ambao ulizinduliwa na Rais John Magufuli hivyo kuwataka wananchi kuwa na subira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles