25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume Njombe washauriwa kusaidia malezi ili kuondoa udumavu

Na Elizabeth Kilindi, Njombe

Wanaume mkoani Njombe wameshauriwa kusaidia malezi kwa watoto kwa kuzingatia lishe bora ili kuondokana na changamoto ya udumavu.

Ushauri huo umetolewa katika mdahalo wa lishe uliofanyika mjini Njombe Desemba 28, 2021 ambapo imeelezwa kuwa changamoto ya udumavu inazidi kutokana na wanaume kujiondoa katika malezi kwa kudhani ni jukumu la mama pekee na hivyo kusababisha tatizo hilo kuzidi kuwepo.

Mkutano huo ulihusisha wazazi na baadhi ya waandishi wa Habari kwa ajili ya kujadili sababu za Mkoa wa Njombe kuendelea kuendelea kuwa kinara kwa udumavu.

Miongoni mwa wazazi walioshiriki mdahalo huo ni Amina Said ambaye alisema suala la malezi kwa mtoto linahusisha baba na mama.

“Nisema tu swala la malezi na kuhakikisha lishe bora kwa mtoto ni la baba na mama lakini inasikitisha kuona mama ndo anaangaika kuhakikisha mahitaji kwa mtoto wakati baba yupo na shughuli zake hii si sawa,” amesema Amina.

Upande wake Aurelia Mtitu amesema kuwa: “Wanaume naomba twende sambamba kwenye hili ili kuhakikisha mtoto anapata afya bora, tukiungana tatizo la udumavu katika mkoa wetu litakua historia,” amesmea Aurelia.

Naye, Emilia Msafiri alisema wamama wamekua wakijikita katika shughuli za kiuchumi badala ya kuweka uangalizi kwa mtoto hali inayosababisha udumavu.

“Ni kweli tunatafuta fedha lakini tujiulize fedha hizi tunatafuta kwa ajili ya nani?unakuta mama anaamka saa 12 asubuhi kwenda shamba nyumbani amemuachia mtoto kande tena za siku tatu huyu mtoto atakua kweli, hiyo lishe bora itakoka wapi tubadilike tuwape hawa watoto mpangilio bora wa chakula,” alisema Emilia.

Kwa upande wa Philoteus Ngilangwa alisema wazazi wengi wanawapa watoto wao chakula ili washibe hali inayosababishwa na ukosefu wa elimu sahihi juu ya lishe.

Hata hivyo, amesema ili kupunguza tatizo hilo elimu itolewe kuanzia ngazi za chini kama mashuleni, vyuoni na kwenye familia, wazazi/walezi wafundishwe namna ya kutumia muda vizuri wa malezi na shughuli za kuwaingizia kipato sambamba na viongozi wa umma walichukue kama ajenda katika vikao vyao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles