30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania waombwa kulipa kodi ya ardhi kabla ya Januari 1

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewaomba Watanzania kulipa kodi ya pango la ardhi kabla ya Januari Mosi mwakani lengo likiwa kuepuka riba ya asilimia moja ambayo watatozwa kila mwezi kama faini endapo mtu atachelewa kulipa kodi hiyo.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Desemba 30,2021 jijini Dodoma na Kamishna wa Ardhi wa wizara hiyo, Nathaniel Nhonge, wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kodi ya pango la ardhi.

Kamishna Nhonge amesema Watanzania wengi wameitikia wito wa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa mwaka huu, hivyo amewataka kuendelea kulipa kwani ifikapo Januari 1, 2021 watatakiwa kulipa faini ya riba ya asilimia moja kwa mwezi.

“Kwa maana ikifika tarehe moja  mwezi wa kwanza kwa maana ile kodi yako inaanza na riba sisi msisitizo wetu ni kilipa kipindi hichi cha miezi sita ambayo haina riba sasa kila mwezi sasa inaanza kuongezeka tunaona ni muhimu kuwaambia wananchi muda upo baada ya tarehe 31 tutaanza kutoza na riba,”amesema Nhonge.

Aidha, Nhonge amesema wizara hiyo imeweka utaratibu mzuri ili kuhakikisha wanatoa huduma bora za ulipaji kodi ambapo wameanzisha kituo cha mawasiliano kwa wateja na wanaweza kuwahudumia wananchi popote walipo ili kuwawezesha kulipa kodi.

Vilevile amesema mikakati ya wizara hiyo ni kuhakikisha ina pima ardhi kwa kasi ili kila Mtanzania aweze kumiliki ardhi ambapo tayari wizara hiyo ilishapokea fedha kiasi  cha Sh bilioni 50 kutoka serikalini kwa ajili ya kazi hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha kodi cha wizara hiyo, Denis Masami, amesema kuwa katika kipindi cha kuelekea mwisho wa mwezi mwitikio wa ulipaji kodi ya pango la ardhi umeongezeka na wengi wamejitokeza kulipa.

Amesema hadi sasa wameshakusanya Sh bilioni 60 na malengo ni kukusanya bilioni 221.

“Sasa hivi ukusanyaji umeongezeka kwa wiki tunakusanya  bilioni 2 mpaka 4  kwa Jiji la Dodoma kwa mwaka huu kulikuwa na wamiliki 250 waliokuwa wanalipa lakini sasa hivi wamiliki ni 890 kwa wiki hata kiwango tulichokuwa tunakusanya kilikuwa milioni 60 mpaka 70 sasa hivi mpaka milioni 200.

“Sasa hivi wananchi wanajua na wanaona ni vyema kulipa kodi lakini ni pamoja na mikakati ambayo tumekuwa tukiweka.Mwitikio kwa sasa ni mkubwa wengi wamelipa,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles