25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi ya UKIMWI kwa watoto yapungua Bukoba

Renatha Kipaka, Bukoba

Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 0-14 Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera yamepungua kutoka asilimia 4.0 kwa mwaka 2020 hadi kufikia 1.5 Septemba mwaKa 2021.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa UKIMWI wa Manispaa ya Bukoba, Samweli Chaba, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapo.

Chaba amesema kuwa kwa mwaka 2020 kuanzia Januari hadi Septemba watoto 700 walipimwa VVU ambapo wavulana walikuwa 3313 na wasichana 387.

Amefafanua kuwa kipindi cha mwaka 2021 walipimwa watoto 1,664 ambapo wavulana walikuwa 718 na wasichana 946 kutoka Januari hadi Septemba.

Mratibu huyo amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2020 waliokuwa na maambukizi ni watoto 28 kati ya waliopimwa kipindi hicho ambapo wavulana ni 13 na wasichana 15 na walianza matibabu wote sawa na asilimia 100.

“Kwa mwaKa 2021 tulibaini watoto 25 kati ya waliopimwa kipindi hicho wavulana 15 na wasichana 10 na wote walianza kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI hii nisawa na asilimia 100,” amesema.

“Niseme ndugu zangu matokeo ya kupungua kwa maambukizi ya Ukimwi kwa watoto nikutokana na elimu inayotolewa na wataalamu wa Afya kwa wazazi na walezi juu ya kujikinga ili wasipate maambukizi lakini pia ambao wameshaambukizwa wanatumia dawa kwa usahihi”amesema Chaba

Aidha Mratibu huyo amesema kuwa mama anayeishi na virusi vya Ukimwi anapofuata mashariti na kutumia dawa kwa usahihi anaweza kubeba mimba na kuzaa mtoto asie na maambukizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles