23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume China walipa kina mama kunyonya maziwa yao

1

UNYONYAJI wa maziwa ya mama kwa watu wazima umekuwa soko linalokua kwa kasi nchini China, lakini pia likitiwa doa na wenye malengo tofauti na hilo.

Nchini China, kutokana na imani kwamba maziwa ya mama yana virutubisho vya uponyaji, biashara hiyo imekuwa ikikua kwa kasi. Hii ni kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post.

Watu wazima iwe wanaume au wanawake wanawalipa wanawake fedha ili wanyonyeshe maziwa yao kutoka kifuani mwao.

Kuna aina nyingi za malipo ambapo, kwa mfano kuna vituo vinavyoendesha huduma vikiwa vinajitangaza kupitia tovuti.

Mteja anaweza kujiunga katika kituo akilipa ada ya uanachama ya dola 10 sawa na Sh 21,000 kisha hutakiwa kulipa kwa mwezi kuanzia dola 3,000 hadi 5,000 sawa na Sh milioni 11 kwa mwezi.

Hilo huwaruhusu kwenda kuyanyonya maziwa hayo moja kwa moja kutoka vifuani mwao kwa kadiri ya muda wao ndani ya mwezi ikiwa ni tofauti na wale wa malipo ya papo hapo.

Watu wengi wanaona jambo hilo ni la ajabu kwa mwanamume au mwanamke mzima kunyonya matiti ya mwanamke mwenzake.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni maradhi. Wengi wao ni wale wenye magonjwa sugu na ambao wanashindwa kupata chakula chenye virutubisho bora vya asili kwa vile vyakula vingi nchini humo vimechakachuliwa.

Hivyo, kwa kuishi katika mazingira ambayo vyakula vimechakachuliwa, watu hukimbilia maziwa ya kinamama ambayo wanaona ndicho chakula halisi na cha asilia na chenye viini vingi vyenye kuimarisha afya ya binadamu.

Mbali ya kwamba kuna wanaofanya kitendo hicho kama burudani, msingi wa kitendo hicho ulikuwa kuokoa maisha yao, jambo ambalo linafanya kikubalike zaidi.

Watetezi wake wanatupia lawama wale wanaofanya kinyume na malengo haswa ya unyonyeshaji watu wazima.

Ni baada ya watu 15 kukamatwa nchini humo wakishitakiwa kwa ukahaba kutokana na kubainika moja ya tovuti inayotoa huduma hiyo ya kunyonya maziwa kwa watu wazima pia inahusisha ofa ya ngono kwa wanaolipa.

Kwa mujibu wa gazeti la International Business Times, uchunguzi wa hivi karibuni wa polisi ulisababisha kufungwa kwa moja ya tovuti hizo. Ni baada ya kubainika kwamba wamiliki wake walitoa mara kwa mara kazi hiyo kwa wale wanawake ambao walikubali pia kutoa huduma za ngono mbali ya kunyonywa maziwa.

Tovuti hiyo iliwasiliana na wateja wake kupitia programu maalumu za ujumbe wa maandishi na kutoa picha za kina mama wa kuchagua.

Genge hilo lilifichuliwa baada ya mwandishi mmoja wa uchunguzi kujifanya mteja wa kunyonya maziwa kupitia tovuti hiyo na aliripotiwa pia kupewa ofa ya ngono.

Alilipa pauni 133 za Uingereza sawa na zaidi Sh 390,000 pamoja na ofa ya ngono ya pauni 155 sawa na Sh 450,000.

Aidha, Lin Jun, mmiliki wa kampuni ya huduma ya Xinxinyu, ambayo pia inatoa huduma za kunyonya maziwa aliliambia International Business Times kuwa wateja wanaweza kunywa maziwa moja kwa moja kutoka kifuani mwa mama au kupitia pampu iwapo wanaona haya kunyonya.

Lakini pia maziwa ya mama yamekuwa anasa mpya kwa matajiri wa China.

2

Wamama wanaotoa huduma hiyo wamekuwa maarufu kuliko wakati wowote huo kihistoria, wakitoa maziwa si kwa vichanga tu bali pia wagonjwa na matajiri wanaoamini kwamba maziwa hayo ni bora zaidi na rahisi kuwapatia virutubisho vitakiwavyo.

Kwa mujibu wa tafiti, maziwa ya mama yana viinilishe muhimu vya uponyaji.

Kwa mfano; kama ilivyoripotiwa na Jarida la Medical Daily, maziwa ya mama yanaweza kutibu maambukizi ya macho na sikio.

Hilo linatokana na wingi wa kinga asilia za mwili uliopo katika maziwa. Pia iliripotiwa kwamba kinga hizo hizo zinaweza kuponya vidonda vya koo na kuondoa mwasho wa ngozi.

Aidha, kwa mujibu wa jarida la Discover, kuna utafiti unaofanyika kuangalia kama maziwa ya mama yanaweza kutoa kinga dhidi ya saratani.

Hata hivyo, wakati manufaa ya maziwa ya mama yakiwa wazi, matumizi ya maziwa hayo kunyonyesha watu wazima ni suala linalowagawa wengi.

Baadhi wanahisi kuwalipa mama wapya na mara nyingi masikini kwa ajili ya maziwa yao si tu ni kuwadhalilisha wanawake hao bali pia tusi kwa dhana nzima ya umama.

Pia ili kuwa na maziwa ya kutosha kuwalisha wanaume watu wazima, kina mama mengi watalazimika kutokuwa na maziwa ya kuwalisha watoto wao.

“Hilo linaongeza tatizo juu ya tatizo nchini  China; kuwahesabu wanawake kama bidhaa na ni ushuhuda wa kushuka kwa maadili miongoni mwa matajiri wa China,” anasema Cao Baoyin, mwandishi na mchambuzi katika vyombo mbalimbali vya habari vya China.

Wengine wanaona hakuna kosa kuchagua kunyonya maziwa ya mama iwapo yanachukuliwa kutoka kwa kina mama ambao matiti yao yamejaa maziwa ya kutosha.

Watetezi wa kitendo hicho hawako China tu, bali hata katika mataifa ya magharibi.

“Nataka kitu cha asili kilichotolewa na Mungu. Ni sawa kwa mama wanaotaka kuyapunguza, nitayachukua,” alieleza Anthony, mjini New York Marekani.

Naye Wendy Haldeman, mwanzilishi mwenza wa kituo cha unyonyeshaji maziwa ya mama huko Santa Monica, California anasema:

“Si ajabu kwa watu wazima kutafuta maziwa ya mama. Nawafahamu wanaume fulani wenye saratani wanaokunywa maziwa ya mama kama sehemu ya matibabu,” Haldeman alisema.

Hilo linawafanya wanaume wa magharibi wapate kisingizio cha kunywa maziwa ya mama. Kwa wakati fulani baba wengi wapya hujaribu kuonja.

Wakati kulipa kwa ajili ya ngono ikiwa ni kosa nchini China, usambazaji wa maziwa ya mama unaonekana kukubalika na hivyo kuzidi kuwa maarufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles