32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wanaogeuza dili kusajili watoto kukiona

Waziri wa Katiba na Sheri, Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Katiba na Sheri, Harrison Mwakyembe.

NA RAYMOND MINJA -IRINGA

SERIKALI imetangaza kuwaweka  kikaangoni na ikiwezekana kuwafuta kazi maofisa wa Serikali na watendaji wanaogeuza dili mchakato wa usajili wa watoto katika daftari la vizazi na vifo ilhali wanalipwa mishahara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa usajili na kutoa vyeti kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Iringa na Njombe, Waziri wa Katiba na Sheri, Harrison Mwakyembe, aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kutowafumbia macho maofisa na watendaji watakaobainika kufanya ubadhirifu huo  ili nao walinde vibarua vyao.

Mwakyembe alisema  kumekuwa na  tabia ya watendaji na watumishi wa Serikali kugeuza kila kifanyikacho  hapa nchini kuwa ni fursa ya kupiga dili hata kama jambo lenyewe ni la bure.

“Tatizo la nchi hii, kila kitu watu wanageuza dili hata vitu ambavyo havifai kuitwa dili, sasa katika hili la usajili wa watoto nitakwenda nao sambamba, yeyote atakayechukua fedha za wananchi ili kuwaandikisha au kumwandikisha mtu ambaye si Mtanzania,” alisema.

Mwakyembe alisema ni vyema kila mmoja akafanya kazi kwa kufuata misingi na taratibu za nchi na kuwataka watendaji kuhakikisha wanawaandikisha watoto wote, idadi kamili ya watoto walioko chini ya miaka mitano ipatikane ili iwe rahisi kwa Serikali kuhudumia watu wake pindi wanapokuwa na uhitaji.

Akizungumzia hali ya uandikishaji, Mwakyembe alisema kwa mujibu wa utafiti wa idadi ya watu nchini ya mwaka 2010, ni asilimia 16 tu ya watoto walio chini ya miaka mitano walikuwa wamesajiliwa na mamlaka za Serikali, huku akiitaja mikoa  ya Iringa na Njombe kuwa ni mikoa iliyo nyuma katika usajili wa watoto.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Rita, Profesa Hamisa Dihenga, alisema hali si shwari katika usajili kwani takwimu za mwaka 2012, zinaonyesha ni asilimia 13.4 tu ya Watanzania bara wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles