Adhabu ngumu zitungwe kukomesha ujangili

0
530

temboo-798x350

NA AMON MTEGA –  TUNDURU

MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera, amesema wakati umefika kwa Serikali kutunga sheria na adhabu ngumu kwa watu watakaobainika kufanya vitendo vya kijangili.

Homera aliyasema hayo juzi wakati akitoa salamu za wilaya hiyo pamoja na changamoto zinazowakabili wakazi wanaoishi karibu na maeneo ya mapori ya hifadhi kama Selous, kwenye maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa yaliyofanyika wilayani hapa.

Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Utunzaji wa Mazingira Duniani (WWF).

Homera alisema majangili wamekuwa wakifanya vitendo haramu kwenye mapori hayo kwa kuwaua wanyama hasa tembo kwa masilahi yao, hivyo wakati umefika kwa Serikali  kutunga sheria ngumu pamoja na kuweka adhabu itakayosaidia kuwaokoa wanyama hao wasiendelee kuteketea.

Mkuu huyo akitoa salamu za wilaya hiyo, alisema licha ya Serikali kufikiria namna ya kutunga sheria hiyo, lakini bado Wizara husika ya Maliasili na Utalii pamoja na WWF wakae meza moja  na kuangalia namna bora ya kudhibiti wanyama waliopo kwenye hifadhi ili wasiende kwenye makazi ya binadamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here