21.4 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wamlilia Diwani kuiomba Serikali kupunguza bili za maji

Na Sheila  Katikula, Mwanza

Katika kipindi hiki cha janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), Diwani wa kata ya Nyamagana iliyopo jijini Mwanza, Bhiku Kotecha amekiri kufuatwa na wananchi wakimuomba awafikishie ujumbe wao kwa serikali  iweze kupunguza bili za maji ili waendelee kunawa na kujikinga na Korona.

Kotecha ameeleza hayo katika mahojiano maalumu na mtanzania digital ambapo alieleza kupokea malalamiko katika kipindi hiki cha janga la tatu la maambukizi ya virusi vya Korona wakieleza kushindwa kumudu gharama za maji kwani ni kiwango kikubwa sana cha maji kinatumika.

Amesema wananchi wa kata hiyo wamesema wamehamasika kujikinga na UVIKO-19 ili kuunga mkono juhudi za serikali lakini suala la gharama za maji limekuwa kikwazo cha wao kujikinga na ugonjwa huo hivyo ni vema serikali kupunguza  bili ili watu waweze kutumia maji bila wasi wasi.

“Wananchi wa kata yangu wameniagiza niwasemee kwa  serikali hususani wizara ya maji kuangalia ukubwa wa tatizo lililopo nchini la ugonjwa wa UVIKO-19 kwani maji yanatumika  kwa asilimia kubwa  kwa ajili ya kunawa wamikono ikiwa ni njia ya kujikinga kutokana na maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya”,alisema Kotecha.

Hata hivyo amewaomba  wananchi wajitokeze kwa wingi kuendelee kupata chanjo kwani ni salama na haina tatizo lolote  sanjari na  kuacha  kusikiliza maneno ya upotoshaji ya kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha hofu ambayo haina tija katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles