24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaka aitaka TALGWU kutetea maslahi ya wafanyakazi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka amekitaka Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kuhakikisha kinaendelea
kutetea maslahi ya wafanyakazi pamoja na kuwaandaa watumishi wa umma
kujua wanatakiwa  kufanya nini mara baada ya
kustaafu.

Akizungumza leo Jumanne Agosti 24, jijini Dodoma katika mkutano Mkuu wa TALGWU, Mtaka ametoa wito kwa chama hicho kuendelea kutetea maslahi ya wafanyakazi nchini kwenye mambo ya msingi.

“Wito wangu kwenu tusimamie maadili ya watumishi tuwatete kwenye mambo
ya msingi hata kwenye gharama za kesi fanyeni zile zenye mantiki ili
muache alama,”amesema Mtaka.

Aidha, amekitaka chama hicho, kuwaandaa watumishi kabla ya kustaafu ili
wajue wanatakiwa kufanya baada ya kustaafu kwani baadhi
wamekuwa wakitapeliwa baada ya kustaafu.

Pia amewataka kuwa na malengo yanayoishi ikiwemo kuweka vitega
uchumi ambavyo vitawasaidia katika kujiendesha.

“Lazima muwe na malengo mnayoyaishi sio muda wote mpo mahakamani hii
inaharibu tengenezeni vitu vizuri ambavyo vitawaonesha,” amesema Mtaka.

Katika hatua nyingine, Mtaka amekielekeza chama hicho kuwapa maelezo ya kutosha watumishi wapya ili wajue
umuhimu wa chama hicho kwani wengi wamekuwa wakidanganywa kuhusiana na chama hicho.

“Hawa wanaoajiriwa wanasema chama cha nini hakuna ambaye ameelimishwa
kuhusiana na Bima na Pension lakini lazima kuwe na utaratibu wa kufanya semina hii itasaidia sana,” amesema Mtaka na kuwahimiza kuwekeza ,mkoani humo katika sekta ya ardhi
kwani kuna fursa nyingi.

“Hapa ni makao makuu ni kama unavyoenda Dar es Salaam unakuta mtu ana hekari mbili
Mikocheni unajiuliza alipataje. Nawaomba pata muda, Dodoma chumba na
sebule ni Sh 200,000 si kitu kibaya huu muda ambao mpo hapa mpate ka ardhi
kadogo,”amesema.

Akitoa neno  la shukrani Mwenyekiti wa TALGU Mkoa wa Mara, Dk. Magreth Shawu amesema wataendelea kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wafanyakazi ili wasikope mikopo inayoumiza.

“Kwa niaba ya wafanyakazi tunashukuru yapo mengi umetuasa kikubwa umetuasa tuwe watumishi tunaosikiliza na kusimamia. Tunaenda kufanya uchaguzi ambao utakifanya chama chetu kiwe imara zaidi. Tunakuahidi sisi kwa kuanzia katika ngazi za mikoa tutaenda kulisimamia suala la utoaji wa elimu kwa watumishi wenzetu wasiharibiwe na mikopo umiza,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles