25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Wananchi wampa kibarua Meneja wa Tanesco

Abdallah Amiri – TABORA

BAADHI ya wananchi wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora wamemlalamikia Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Wilaya ya Igunga,  Jamal Kimoro kwa kushindwa kutatua tatizo la kukatika umeme mara kwa mara katika wilaya ya Igunga.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika maegesho ya malori na Stendi Kuu ya Mabasi mjini Igunga baadhi ya wananchi hao Moka Changarawe, Hassan Jumanne,  Ashura Jumbe, na Rajab Juma.

Wamesema hivi sasa wanashindwa kufanya shughuli za uzalishaji kutokana na kukatika katika umeme kila siku zaidi ya mara nne.

“Kwa kweli kukosekana kwa umeme mara kwa mara maisha yetu yamekuwa magumu sana wanaigunga” alisema.

Changarawe alibainisha kuwa yeye anajishughulisha na uzibaji wa pancha katika maegesho ya malori lakini hivi sasa hafanyi kazi kutokana na kukosekana nishati hiyo ya umeme.

Aidha Ashura alisema hivi sasa biashara ya soda, juice hawauzi kutokana na kukosekana umeme mara kwa mara huku akiongeza kuwa endapo tatizo la kukatika kwa umeme halitapatiwa ufumbuzi wafanyabiashara wengi watashindwa kurejesha mikopo yao waliyokopa benki.

Kutokana na hali hiyo wamemtaka Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya ya Igunga kufuatilia suala hilo kwa haraka ili waweze kubaini kukatika kwa umeme katika wilaya ya igunga mara kwa mara.

Akijibu hoja hizo Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya ya Igunga, Jamal Kimoro alipoulizwa juu ya malalamiko ya wananchi ya kukatika umeme mara kwa mara alikiri kuwepo tatizo hilo.

“Ni kweli umeme umekuwa ukikatika kila mara hata hivyo bado tunafuatilia kila eneo ili kujua tatizo hilo na tukishagundua nitatoa taarifa,” alisema Meneja huyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles