27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Papa Francis ataka umoja kukabili corona

REME, ITALIA

Papa Francis ametoa wito wa mshikamano kote duniani katika kukabiliana na virusi vya corona kwenye ujumbe wake wa kuadhimisha Jumapili ya Pasaka.

“Huu sio wakati wa kutofautiana. Kwasababu dunia nzima inataabika na inachohitaji ni kuungana,” Papa amesema hivyo katika ujumbe uliopeperushwa moja kwa moja mtandaoni, kutoka katika kanisa la mtakatifu Petro.

Alionya kwamba kuna hatari ya Muungano wa Ulaya kuvunjika na kutoa wito wa kusamehewa kwa madeni kwa nchi masikini.

Ibada za ya Pasaka zimefanyika bila kuhudhuriwa na watu makanisani sehemu mbalimbali duniani wakati ambapo mamilioni ya watu wametakiwa kusalia majumbani.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alitoa baraka zake kwa mji wa Roma na dunia nzima huku amri ya kusalia ndani ikiendelea kudumishwa nchini Italia, moja ya nchi iliyoathirika vibaya na janga la Corona.

Alisema kwamba ujumbe wa pasaka wa mwaka huu ambao umekuwa wa upweke, unatakiwa kuwa wa matumaini, na kusihi viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa manufaa ya wote, kusaidia watu katika kipindi hiki kigumu na hatimaye kurejea katika maisha ya kawaida.

“Huu sio wakati wa kuwa wabinafsi kwasababu changamoto iliyopo inakabili kila mmoja,” Papa alisema katika ujumbe wake uliojikita zaidi katika athari za mlipuko wa ugonjwa wa corona ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 109,000 kote duniani.

“Kutojali, ubinafsi, migawanyiko na usahaulifu ni maneno ambayo hatutaki kuyasikia kipindi hiki. Maneno haya tunataka kuyakomesha milele,” aliongeza.

Bila ya kutaja nchi yoyote, Papa pia alitoa wito wa kulegezwa kwa vikwazo vya kimataifa na kusifu madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine ambao wanaendeleza huduma za msingi.

Juzi Jumamosi Papa Francis aliwataka watu kutosalimu amri kwa uoga wa virusi vya corona, na kuwataka kuwa “wajumbe wa uhai wakati wa kifo”.

Papa alirejelelea maandiko ya bibilia kuhusu mwanamke ambaye hakumkuta hata mtu mmoja katika kaburi la Yesu siku ambayo Wakristo wanaamini alifufuka.

“Wakati huo pia, kulikuwa na hofu ya siku zijazo na kwamba kutakuwa na haja ya kuanza upya. Kumbukumbu ya huzuni, na kukatizwa kwa matumaini. Kwao, kama ilivyo kwetu, ilikuwa saa ya giza,.

“Msiwe na hofu wala msiogope: Huu ni ujumbe wa matumaini. Tumeupokea leo hii,” alisema Papa

Ibada yake, ambayo kawaida hufanyika mbele ya maelfu ya waumini, ilihudhuriwa na watu kumi na kitu tu. Tamaduni kadhaa za ibada za kanisa hilo pia hazikufanyika ikiwemo ubatizo wa watu waliobadili dini a kuingia katika Ukatoliki.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles