25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Spika atoa neno kwa wanawake kuwania uongozi

KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR

VYAMA vya siasa nchini, vimeshauriwa kuweka na kutekeleza sera maalumu ambayo itakayoweza kutoa fursa kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akitoa hamasa hivyo mjini Unguja, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, alisema   bado kuna changamoto kubwa katika vyama vya siasa ambavyo havitoi fursa sawa kwa wanachama wake wanapotaka kugombea nafasi za uongozi.

Alisema vyama vya siasa licha ya kunadi uwepo wa sera ambazo zinawezesha wanawake katika kugombea nafasi za uongozi lakini sera hizo hadi sasa zimekua zikibaki kwenyer makaratasi na kushindwa kufanyiwa kazi.

“Kuna nafasi za viti maalumu kwa wanawake, hizi ni nafasi za mfano za kuwajengea uwezo wanawake nao kuwa na uthubutu wa kuingia katika michuwano ya majimbo na sio kubweteka wakiamini kuwa hawawezi,” alisema Mgeni

Alisema kuwa licha ya uwepo wa mwamko kwa baadhi ya wanawake kutaka kugombea nafasi za uongozi lakini hadi sasa wengi wao bado hawafahamu nini wanachokitaka na kwanini.

“Ili tuweze kufanikiwa ni lazima sisi wanawake tuweke malengo yetu kabla ya kuingia kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi ili tuweze kumshinda adui yetu,” alisema

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kiwengwa, Asha Abdallah Mussa (CCM), alisema wanawake wanaotaka kugombea nafasi za uongozi wana wajibu wa kufanya utafiti pamoja na kutengeza ushawishi kwa vitendo kwa wajumbe wenye kutoa maamuzi ndani ya chama.

Pia alitoa ushauri kwa Chama cha wanahabari Wanawake Tamwa-Zanzibar,  muda ukifika wa kufanya kampeni kuwaandaa wanawake ambao wanahisi wana mwelekeo wa kukubalika kwenye jamii.

Asha alikiri kuwa kuna tatizo kubwa hususani Zanzibar la wanawake wengi kushindwa kujitokeza katika uchaguzi kutokana na hofu ya kupambana na wanaume kwenye kinyanganyiro.

Kwa upande wake Mwenyekiti Baraza la Wanawake Chadema Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mwanamrisho Abama, alisema ipo haja kufanyiwa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa na kuweka wazi uwepo wa nafasi za wanawake katika majimbo na si kwa nafasi za viti maalumu pakee.

Kwa upande wake Mtunza Hazima wa ACT Wazalendo, Jimbo la Malind, Halima Ibrahim alisema miongoni ipo haja ya wanawake kwenye vyama vyao kuhakikisha wanakua wajumbe wa kamati zenye uwezo wa kutoa maamuzi ya mwisho ndani ya chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles