25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi washindwa kwenda shule kuhofia kuawa na tembo

Safina Sarwatt, Mwanga

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro wameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), kuyadhibiti makundi ya tembo kutoka hifadhi ya Taifa ya Tsavo ambayo yamevamia makazi ya watu na kuharibu mazao.

Hayo yamebainishwa jana Februari 16, na Diwani wa Kata ya Kwakoa, Kiende Mvungi, katika mkutano wa Baraza la Halmashauri ambalo llijadili taarifa za Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika kata kwa kipindi cha Robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2020/2021.

Amesema wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Kwakoa, wameshindwa kwenda shule kutokana na makundi ya tembo kutoka hifadhi ya Taifa Tsavo nchini Kenya.

“Wanafunzi wa wanaosoma katika shule ya Msingi Kwakoa wameshindwa kwenda shule kutokana na kuhofia kuawa na makundi haya ya tembo,” amesema Mvungi.

Naye Diwani wa Jipe, Dk. Ally Kidaya, amesema suala la tembo limekuwa Ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Kata ya Jipe, jambo ambalo limechangia baadhi ya wananchi hao kulazimika kuyakimbia makazi yao.

“Tembo hawa wanavuka kutoka Kenya kuja kuharibu mazao kwa kiwango kikubwa, wananchi wa maeneo haya wamekuwa wakilazimika kuyakimbia makazi yao,” amesema.

Akichangia hoja hiyo Diwani wa Kata ya Toloha, Palesio Makange, amesema makundi hayo ya tembo yamekuwa tishio kubwa kwa wananchi kutokana na kuvamia mazao ya wananchi na kusababisha uharibifu mkubwa na kuziomba Mamlaka husika kuangali namna ya kuwadhibiti ili wananchi waendelee kuishi kwa amani.

“Wako baadhi ya wananchi wamedhurika kutokana na wanyama hawa hivyo tunaiomba serikali iangalie namna ya kuwafidia wananchi hawa,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Zefrin Lubuva, pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Salehe Mkwizu, wamesema, Hlmashauri imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mamlaka za usimamizi Wanyamapori ili kuwadhibiti wanyama hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles