27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Wanafunzi UDOM watakiwa kuripoti chuoni wakichukua tahadhari ya corona

Ramadhan Hassan -Dodoma

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dodoma wametakiwa kuripoti kesho huku wakitakiwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kuhusu kujikinga na virusi vya corona.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee, ilieleza wanafunzi wote wanatangaziwa kuwa chuo kitafunguliwa Ijumaa huku masomo yakianza rasmi Jumatatu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanafunzi wote wanataarifiwa kwamba usajili utaanza asubuhi siku ya Ijumaa hadi Jumapili.

“Wanafunzi wanashauriwa kuzitumia vizuri siku hizi tatu kukamilisha taratibu zote zinazohusu usajili  na malazi kabla ya kuanza kwa masomo  tarehe 1 Juni 2020,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanafunzi wa Ndaki ya Sayansi za Afya (CHS) wanaofanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali za rufaa mikoa ya Iringa na Shinyanga  waende moja kwa moja kwenye vituo vyao vya mafunzo kwa vitendo ambako pia watasajiliwa.

“Wanafunzi wote wanakaribishwa na wanahimizwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kujikinga na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa corona,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles