24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Wanafunzi kidato cha pili waanza mitihani

dk-charles-e-msondeNa Jonas Mushi, Dar es Salaam

BARAZA lA Mitihani Tanzania (NECTA) limesema wanafunzi 397, 250 wa kidato cha pili wameanza kufanya Mitihani ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) ikijumuisha wavulana 197,452 sawa na asilimia 49.70 na wasichana 199,798 sawa na asilimia 50.30.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema mitihani hiyo ilianza jana katika shule za sekondari 4,764 za Tanzania bara na itamalizika Novemba 27 mwaka huu.

Aidha alisema mitihani ya upimaji pia itafanywa na wanafunzi wa darasa la nne ambao wanatarajia kuanza mitihani yao Novemba 25 na kumalizika Novemba 26 mwaka huu.

“Mitihani ya upimaji kwa kidato cha pili husaidia kupima uwezo na uwelewa wa wanafunzi katika yale yote waliyojifunza kwa kipindi cha miaka miwili na kwa upande wa darasa la nne huwezesha kujua kiwango cha wanafunzi katika kumudu stadi za juu za kusoma, kuandika na kuhesabu, ” alisema Dk Msonde.

Alisema mitihani hiyo pia hubainisha maeneo muhimu yanayohitaji kufanyiwa maboresho katika vitendo vya ufunzaji wa wanafunzi waendeleapo na masomo yao ya ngazi za juu.

Mitihani ya darasa la nne itahusisha wanafunzi 1,036, 694 waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo katika shule za msingi 16, 656 za Tanzania bara ikijumuisha wavulana 501,714 sawa na asilimia 48.60 na wasichana 534,980 sawa na asilimia 51.60.

Kuhusu alama za ufaulu katika mitihani hiyo alisema kwa kidato cha pili zinatumika zilezile za mitihani ya taifa ya kidato cha nne ambazo ni alama 30 kwa kila somo huku alama za dasara la nne zikiwa sawa na zile za darasa la saba yaani alama 21 kwa kila soma.

Dk. Msonde alitoa wito kwa wasimamizi wa mitihani hiyo kwa kuwataka kuzingatia taratibu za ufanyaji wa mitihani, huku akiwatahadharisha wanafunzi na wasimamizi hao kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles