29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wamlipa Ngariba kondoo kuzuia watoto wasikeketwe

CHRISTINA GAULUHANGA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Health Integrated Multisectoral Development (HIMD), Macrine Lumanyika amesema walilazimika kulipa kondoo wawili kwa kila ngariba katika jamii za kimasai ili Kuzuia vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Internews  kupitia Mradi wa Paza Sauti kwa kushirikiana na asasi ya kiraia ya Health Integrated Multisectoral Development (HIMD), Macrine amesema, ngariba hao 69 walikubali kutupa visu vyao na viwembe chini endapo watapewa kitu mbadala.

“Kwakuwa hiyo ilikuwa ni shughuli yao walikuwa wakilipwa ujira tulilazimika kuwalipa mangariba hao kondoo wawili kila mmoja ili apate mtaji wa kufuga,”Amesema Macrine.

Ametaja Mikoa ambayo inaongoza kwa ukeketaji ni pamoja na Manyara, Singida, Dodoma, Arusha na Mara ambapo kwa kuanza kampeni hiyo imeanzia Mikoa ya Kaskazini.

Kwa upande wake, Kiongozi wa jamii ya Kimasai, Isack amesema Jambo Hilo likiendeshwa kwa uwazi linaweza kuisha na kwamba yeye binafsi watoto wake wote wanne hajawafanyia vitendo hivyo kwakuwa alitambua madhara yake tangu mwanzo.

“Kitendo cha kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kumfundisha awe na nidhamu na asijiingize kwenye vitendo vya uhuni lakini inaharibu kila kitu inahitaji kuzungumza taratibu ili liishe kwani lina madhara,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles