27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene aagiza vibali vya zamani kufutwa

brighiter Masaki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene amemuagiza Katibu Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuta vibali vyote vya zamani vya wafanyabiashara wa vyuma chakavu.

Simbachawene amesema kuundwe tume ambayo itasimamia utengenezaji wa vibali vipya vitakavyokidhi matakwa ya kibiashara.

Ametoa agizo hilo leo Septemba 4, jijini Dar es salaam  wakati akiongea na wafanyabiashara wa Vyuma chakavu ambapo amesema vibali vyote vilivyotolewa awali vimefutwa na utaratibu wa kuboresha vibali hivyo utafanyika upya ndani ya siku Saba.

“Kamati iundwe ndani ya masaa 24 na iweze kufanya kazi kwa siku saba kukamilisha hivyo vibali vipya, Nemc muwasikilize wafanyabiashara na kuzingatia ukusanyaji wa tozo ili kukuza uchumi wa nchi.”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles