23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli awataka wadau sekta ya ujenzi kuchangamkia fursa

Anna Potinus, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuchangamiia fursa mbalimbali na kuwa na uthubutu wa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania ili kufika mbali zaidi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatano Septemba 4, katika mkutano wa wahandisi na wadau wa sekta ya ujenzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Niwaombe wadau wa sekta ya ujenzi tuchangamkie fursa zaidi ya hapo kuweni na ujasiri wa kuthubutu kutafuta fursa nyingine nje ya mipaka yetu ikiwamo kwenye nchi za SADC na za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo sisi ni wanachama, hamtoki nje inawezekana ni kwa kutojiamini lakini fursa zipo.

“Makandarasi changamkieni fursa acheni kulalamika sana, sasa hivi nchi yetu inatekeleza miradi mingi ya maendeleo, hata kwenye ujenzi wa zile nyumba za Wizara Dodoma tulitangaza tenda lakini ilikuwa ni shida kuwapata makandarasi wa kujenga nyumba moja na fedha ilikuwa inafahamika ni Sh bilioni moja,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles