31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

WALUHYA WAMJIA JUU ODINGA

NAIROBI, KENYA



VINARA wa muungano wa upinzani wa Nasa kutoka jamii ya Waluhya wametangaza vita ya kisiasa dhidi ya Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga na kuwataka wafuasi wao kukikataa chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2022.

Wakihutubia mikutano ya hadhara katika vituo kadhaa vya biashara katika Kaunti ya Vihiga, Kiongozi wa chama cha Ford Kenya, Moses Wetang’ula na mwenzake wa ANC, Musalia Mudavadi, walisema Odinga ameikosea heshima jamii ya Waluhya kwa kuisaliti na kuitelekeza.

Walitaja hatua ya kuondolewa kwa Wetang’ula kutoka uongozi wa wachache katika seneti na wao kudaiwa waoga kuwa ishara tosha ODM ‘imeidharau’ jamii ya Waluhya.

“Mliona namna alivyotukwepa na kwenda kuzungumza na Rais Uhuru Kenyatta. Na juzi mliona alivyochochea kuondolewa ofisini kwa ndugu yangu Wetang’ula kama kiongozi wa wachache katika seneti.”
“Huyo ni msaliti na sisi kama jamii ya Waluhya tukiepuke kabisa na chama chake kinachoshirikiana na Jubilee,” Mudavadi aliwaambia wafuasi wake mjini Mbale bila kumtaja Odinga kwa jina.

Nao viongozi wa ODM wakiongozwa na Katibu Mkuu Edwin Sifuna na Mbunge wa Ugunja, Opiyo Wandayi, waliwajibu kwa kupuuzilia mbali malalamiko yao.

“Watu wanapaswa kuungana kwa masuala yenye umuhimu kwa wananchi kama vita dhidi ya umasikini unaowazonga watu wetu. Si masuala potofu kama kuwashambulia wanasiasa wengine,” alisema Sifuna.
Naye Wandayi alisema: “Hakuna aliyeisaliti jamii ya Waluhya. Hakuna mwanasiasa aliye na uwezo kama huo.

Hili suala la mabadiliko ya uongozi katika seneti linashughulikiwa na maseneta wenyewe, haifa kutumiwa kumchafulia jina kinara wetu Odinga”.

Migawanyiko imeibuka ndani ya NASA baada ya Odinga kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kwa mazungumzo Machi 9 bila kuwahusisha vinara wenzake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles