29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waliosoma Tanga sekondari kuanzisha maktaba mtandao

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Umoja wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Tanga (TSAA) wanatarajia kuanzisha maktaba ya mtandao kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Shule hiyo ya kwanza kuanzishwa wakati wa utawala wa Wajerumani ilijengwa mwaka 1895 ikiwa kituo cha elimu kwa vijana wa kiume na mafunzo ya ualimu na mwaka 1905 iliidhinishwa kuwa shule ya sekondari.

Akizungumza Oktoba 14,2023 Mwenyekiti wa TSAA, Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko, amesema mpango huo unalenga kuinua kiwango cha taaluma katika shule hiyo.

“Umoja huu unalenga kuunganisha nguvu na kuweka jitihada za pamoja katika kuboresha kiwango cha taaluma ikiwa ni dhamira ya kuifanya shule hii kuendelea kutoa wanafunzi bora kitaaluma ili watoe mchango mkubwa katika kulijenga taifa,” amesema Meja Jenerali Semfuko.

Amesema shule hiyo imetoa mchango mkubwa kwa taifa kwa sababu wengi waliosoma wamekuwa watu muhimu ambao wameshika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Amesema kupitia umoja huo wanatarajia kuwaunganisha watu wote waliosoma Tanga School kuanzia miaka ya 1960 mpaka 2022 kwa lengo la kuieneza historia ya elimu ya sekondari nchini kupitia shule hiyo.

Katibu wa umoja huo, Godwin Mbaga, amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu na kwamba kupitia umoja huo wanatarajia pia kuzitatua.

Wanafunzi hao wanatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa kudumu wa umoja huo Oktoba 28,2023 ambapo wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule hiyo akiwemo Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, watashiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles