29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Azam Media yatambulisha Tamthilia ya Lawama

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Azam Media imezindua tamthilia mpya ya ‘Lawama’ ambayo imeelezwa kuwa itaenda kutoa burudani kwa watazamaji wake hususan kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza Oktoba 15, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo Msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza amesema msimu huu unafunguliwa rasmi na tamthilia ya Lawama iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na wapenzi wa tasnia ya filamu nchini.

“Lawama ni moja ya mageuzi makubwa tunayoweza kujivunia kipindi hiki tukisherekea miaka yetu kumi ya huduma kwa kuwa moja ya tamthilia zilizozalishwa kwa teknolojia ya kiwango cha juu na hadithi ya kukidhi mahitaji ya soko la tamthilia ya Tanzania na nje ya mipaka,” amesema Mgaza.

Aliongezea kuwa tamthilia ya lawama ina hadithi ya kuvutia inayojikita kwenye mgogoro juu ya mume kupewa kulea mimba isiyokuwa yake kwa lengo kuu la mke kujipatia mali.

Pia amesema kuanzia Januari 2024, wataanza mchakato wa kupokea filamu kutoka kwa watayarishaji wa kazi za sanaa nchini.

Kwa upande wa mwandaaji wa tamthilia hiyo Brandina Chagula maarufu kama Johari amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani wamejipanga kwa kutoa elimu, burudani kwa kupitia tamthilia ya lawama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles